ukumbusho

🌠TULIKUA TUNAJUA LAKINI HATUTENDI


Barua hii ilinipa tafakari nzito iliponifikia kutoka kwa rafiki yangu mpenzi, na nikapenda watu wote wafaidike na yaliyomo


🌼Amesema Ibn Qayyim: (Alikufa mwanamke kutokana na ugonjwa wa tauni, na baba yake alimuona binti yake kwenye usingizi..Akamwambia: Ewe binti yangu nieleze habari za akhera!! Akamjibu: Tumekuja kwenye jambo kubwa na tulikuwa tunajua lakini hatutendi..wallahi tasbiha moja au rakaa moja katika kitabu cha matendo yangu napenda zaidi kuliko dunia na vilivyomo..

Mwanamke huyu amesema neno kubwa(tulikuwa tunajua lakini hatutendi) lakini wengi wetu hatujui makusudio yake


🌼Tulikua tunajua kusema "subhaana llaahi wabihamdihi" mara mia moja,tunaghufiriwa dhambi zetu hata zikiwa kama wimbi la bahari(na zinatupita siku kadhaa bila kuzisema)


🌼Tulikua tunajua kuwa rakaa mbili za swala ya dhuha zinalingana na siku 360 za kutoa sadaka(siku zinapita na kupita lakini hatuziswali)


🌼Na tulikua tunajua kwamba funga ya siku moja ya sunna katika njia ya Mwenyezi Mungu,Mola humuweka mbali na moto kwa mahandaki saba,na humuweka mbali na moto kwa miaka sabini


🌼Na tulikua tunajua kwamba anayemzuru mgonjwa,hufuatwa na malaika elfu sabini wanamuombea maghfira kwa Mwenyezi Mungu(na hatujazuru wagonjwa wiki yote hii)


🌼Na tulikua tunajua kwamba anayeswalia maiti na akafuata jeneza mpaka akazikwa,anapata ujira wa mfano wa milima miwili ya uhud(na zinapita wiki kadhaa hatujakwenda makaburini)


🌼Tulikua tunajua kwamba anayejenga kwa ajili ya Allah msikiti,hata ukiwa kama kiota cha ndege,Mwenyezi Mungu humjengea nyumba peponi(na hatujachangia kujenga misikiti japo kwa dinari kumi)


🌼Na tulikua tunajua kwamba anayejitahidi kuwahudumia wajane na watoto wao masikini ni kama Mujahid katika njia ya Mwenyezi Mungu,na kama mfungaji mchana ambaye hafuturu,na kama msimamaji usiku wote asiyelala(na hatuchangii kuwadhamini wajane na watoto wao)


🌼Na tulikua tunajua kwamba anayesoma qur-an harufu moja anapata ujira mara kumi(na hatujitahidi kusoma qur-an kila siku)

🌼Na tulikua tunajua kuwa hijja yenye kufanywa kwa uzuri,haina jazaa isipokua pepo,na ujira wake ni kurudi yule aliyehiji kama siku aliyozaliwa na mama yake(yaani anafutiwa dhambi zote) na hatukujitahidi kuhiji pamoja na kwamba uwezo upo na mambo ni mepesi


🌼Na tulikua tunajua kuwa kisimamo cha usiku ni heshima kwa muumini,na kwamba Mtume SAW na Masahaba hawakuacha kuswali qiyaam umri wao wote,pamoja na kuwa wakishughulika kutafuta rizki zao,na kupigana jihad,na kueneza da'wah..ama sisi,tuna mapungufu makubwa katika hili


🌼Tulikuwa tunajua kuwa kiama kitakuja hakina shaka,na kwamba Mola atawafufua walioko makaburini,lakini hatukujiandaa na ujio wa siku hii


Na tulikua tunaswalia maiti na kuwazika,na hatukufanya juhudi kwa siku hii,kama vile tuna shahada inayotuambia sisi hatumo.Jua ewe kaka na dada zangu wapenzi kuwa kila pumzi unayoivuta inakupeleka kwenye mauti..na bado tunacheza na kustarehe


🌼Imeshafika wakati kugeuza mwenendo wa maisha yetu,na tujiandae kikweli kweli na siku ya hesabu(siku ambayo mtu atamkimbia kaka yake,na mama yake na baba yake,na mke wake na watoto wake.Kila mtu siku hiyo ana jambo linamtosha)


🌠Pongezi kwa aliyeyasoma maneno hayo,na akajitahidi kuyatekeleza..na Mola amjazi kheri anayewatumia wengine


      🌰TUAMRISHANE🌰

                    🌰MEMA🌰

Comments