Nissan yaunda magari mapya yanayotumia umeme

No Kampuni ya magari ya Nissan imezindua magari
mapya ya umeme, wakati inakabiliana na
ushindani unaozidi kukua wa magari ya umeme
Aina hiyo mpya ya magari yanaweza kusafiri
mwendo wa asilimia 50 zaidi baada ya kupata
chaji, kwa mujibu wa kampuni hiyo.
Hata hivyo bado magari hayo hayajafikia mwendo
wa magari wa Tesla na GM.
Magari hayo yanayofahamika kama 'Leaf'
yanakabiliwa na ushindani mkali wakati sekta ya
magari yanayotumia umeme inazidi kukua.
Magari mapya ya Leaf yameuzwa nchini Japan
kuanzia Oktoba na yataanza kuuzwa sehemu
zingine mwaka ujao.
Kati ya mabadiliko yaliyofanyiwa hayo magari
hayo ni mfumo wa kujindesha unaofahamika
kama ProPilot Park, ambao huyawezesha
kepenya maeneoimagumu hususan wakati wa
kuegeshwa.

Pia yana teknolojia ya kujiendesha yenyewe hasa
kwenye babara ambayo inaelekea upande mmoja
tu.
Bei ya magari hayo itaanzia yen 3,150,360 au
pauni 22,220.

Comments