MAMA NI MAMA TUMTHAMINI MAMA

*⚜MAMA NI MAMA⚜*
⚜Hata awe kabila gani na sura gani, fukara au mzito wa tabia.
 Huna wala hutopata kama *Mama*.
⚜Waulize watu ambao *Mama* zao walotangulia mbele ya haki.
⚜Kumpenda *Mama* sio kumuweka kwenye "Profile" Eti "I love U Mum, Oooooh I Miss u my Mum", na upuuzi mwingi kuwaonyesha watu.
 ⚜Huna bora duniani zaidi ya *Mama*.
Thamani yake kwako Iko juu kuliko Wanao na Mkeo.
 Na Kiislamu *Mama* ana daraja Tatu juu ya Baba.
⚜Pepo iko chini ya nyao zake, leo upate usingizi hujui *Mamako* amekula nini? Jee ni mzima afya yake? Jee *Mama* anadaiwa?
⚜Kumbuka watu hawashindani kama ndugu zako hawamwangalii *Mama*.
Waache vita vyao na Allah.
Wewe Wajib wako ni umlee kuliko alivyokulea wewe.
Wala huwezi kulipa Fadhla zake hata umfanyie kubwa gani.
⚜Leo imekuwa *Mama* anamuogopa Mwana hata kumwangalia,
Mwana humkaripia *Mamake* kuliko Jibwa lake.
*⚜Subhaanallah*.
Kisha adanganya watu kwa Facebook, I love my Mum, Muwongo mkubwa.
⚜Wee ule Mahunjumati *Mamako* ale chukuchuku.
⚜Wewe ukiwa mgonjwa Agakhan *Mamako* Aljum'ah Dispensary.
Kisha ukhadae watu Aljuma'h ni Private.
⚜Ukimdharau *Mamako* na Mkeo atamdharau na Wanao watampanda utosini na watu wote watamdharau.
⚜Bajeti ulompangia *Mamako* ya mwaka, kwako ni ya wiki moja tu,
 kisha ujisifu unamwangalia *Mamako.*
⚜Unangoja afe uanze vishindo vya Khitma na Mabiriani na kuweka mauwa kaburini.
⚜Mpe uwa akiwa hai aweza kulinusa.
⚜Tumuogopeni Mwenyezi Mungu,

Comments