Magufuli azindua uwanja wa ndegevita Tanzania

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, amezindua uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere uliofanyiwa ukarabati baada ya miundombinu ya uwanja huo kuharibika.
Katika hotuba yake Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Tanzania (JWTZ) kwa kazi kubwa linayofanya na pia akamshukuru Rais wa China Xi Jinping na Serikali yake kwa msaada mkubwa iliyoutoa kujenga uwanja huo.
  • "Mhe. Balozi Lu Youqing naomba unipelekee shukrani zangu za dhati kwa Rais wa China kwa kutoa msaada huu mkubwa wa kujenga uwanja wa ndegevita wa Ngerengere, najua China imetusaidia kujenga Reli ya TAZARA, Kiwanda cha Urafiki na Uwanja wa Mpira, hii yote inathibitisha uhusiano wetu mzuri, urafiki na undugu"
Rais Magufuli akifyatua risasi hewani kuashiria ufunguzi wa uwanja wa ndege vita nchini Tanzania


Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing amesema kujengwa kwa uwanja huo kumeimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na China na amempongeza Magufuli kwa kuendeleza uhusiano huo.
Mbali na kuzindua uwanja huo Magufuli alishuhudia maonesho ya ndege za kivita zilizorushwa kwa mbinu mbalimbali za kivita, ili kutoa heshima

Rais Magufuli azindua uwanja wa ndege vita NgerengereHaki miliki ya pichaIKULU YA TANZANIA
Image captionRais Magufuli azindua uwanja wa ndege vita Ngerengere

Rais Magufuli akihutubia wakati wa ufunguzi wa uwanja wa ndegevita Ngerengere
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo amesema ukarabati wa uwanja huo ulioanza tarehe 15 Julai, 2013 umegharimu Tanzania bilioni 137 na milioni 631 ikiwa ni ufadhili wa Serikali ya China na umehusisha kujenga upya njia ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 3,000 upana wa mita 45 na unene wa sentimeta 45.
Jenerali Mabeyo ameongeza kuwa uwanja huo ni miongoni mwa viwanja bora zaidi duniani kwa sasa na una uwezo wa kutumiwa na ndege za aina zote zilizo chini ya Boeing 777 huku akibainisha kuwa pamoja na ndege za kivita pia unaweza kutumiwa na ndege za kawaida za abiria kwa dharula

Comments