CHEKA UPATE AFYA

Leo mjomba kaja na gari lake nyumbani kumtembelea mshua akaniuliza "hivi *_MOHD_*
  unajua kuendesha gari?? Nikamwambia "ndiyo mjomba najua" akaniambia "chukua hii funguo chukua gari langu nenda ofisini kwangu kanichukulie simu zangu nimezisahau" dah nimefurahi sana nimeona kama ndoto mjomba kunipa gari lake nikajisemea lazima kitaa wanikome

Nimejiandaa fasta fasta nikaaga pale mjomba akaniambia"ufanye haraka sana kuna sehemu tunaenda na baba yako" nikamwambia poa nimeliwasha gari kwa mbwembwe nikaingia nalo kitaa huku nimefungua vioo vyote ili watu wanione vizuri nimeweka sauti ya redio mpaka mwisho
Nimepita sehemu zote ambazo wanapendaga kukaa mademu wa kitaa wamenishangaa vibaya mno hata wale wanaoninuniaga wamenichekea leo

Nimeenda ofisini kwa mjomba pande za posta nikawakuta wafanyakazi wake wakanipa simu zake Galaxy na Blackbery nikatoa line za mjomba nikaweka line zangu ili nikienda kwa mademu wajue simu zangu

Kila sehemu nikiona mademu mara nishuke nitoe Galaxy nianze kujipiga mapicha kwenye gari mara niwaombe mademu nipige nao picha ili mradi tu waione ile Galaxy na Wajue nipo na gari

Nikakumbuka kuna demu nilimtongozaga yupo pale IFM nikampigia simu akaniambia nimfuate chuo nimemfwata hadi chuo na gari amefurahi sana kuniona nimemkuta yupo na rafiki zake kama wanne wamejua mimi mtoto wa kishua sana kuniona nna simu za gharama na gari kali vile yule demu akaniambia "bby tunaomba utupeleke Mliman city hawa wenzangu kuna vitu wanaenda kununua" nikamwambia "usikonde bby twendeni hii gari yangu hata usiwe na wasiwasi bby" nimewapakiza wale mademu tukaanza safari kufika kwenye mataa ya Magomeni nikaona mtu yuko mbele anasimamisha gari kuangalia vizuri namuona Mshua na Mjomba wapo na bodaboda

nimechanganyikiwa balaa nikapaki gari pembeni mjomba kaja kufungua mlango anakuta nyuma nimejaza mademu nimeweka mziki hadi mwisho akaniambia "yani wewe Fuledi mimi nakutuma ukanichukulie simu zangu ofisini wewe umepakia wanawake kwenye gari yangu unatanua mimi na baba yako mda wote huu tunakutafuta tunajua labda upata ajali kumbe unafanya upumbavu"

mshua kanishusha kwenye gari kama kiroba kanipiga mtama wa nguvu nimeangukia kwenye mtaro wa maji machafu kavua mkanda wake kaanza kunitandika mbele za mademu  wa chuo nimepiga kelele nimelia nikaona wale mademu wanaondoka huku wanacheka

 nimeona sana  mshua na mjomba wakaondoka na gari wakaniacha pale nimekaa chini nimelowana matope nalia watu wananishangaa......😆😆😆😆😆😆😆

Comments